Marehemu Edyline Barnabas Mafwere enzi za uhai wake.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
Judith, msichana anayedaiwa kufanya mauaji hayo ambayo yamegeuka kuwa
gumzo mjini hapa, anadaiwa alijaribu kumuua msichana huyo mara ya kwanza
Mei 10, mwaka huu, lakini akashindwa baada ya jirani mmoja kumuwahi na
kumkuta akiwa amemkaba shingo.
Mwenyekiti mstaafu wa serikali ya mtaa huo, Hasda Msuya alisema akiwa
nyumbani kwake, siku hiyo alisikia sauti ya mtoto akilia kwa muda mrefu,
alipokwenda katika nyumba hiyo alimkuta Judith akimpiga marehemu huku
akiwa amemkaba shingo, lakini akamkemea na kuondoka zake.
Mama mzazi wa Edyline Barnabas Mafwere akilia kwa uchungu.
“Jana (Mei 20, 2015) majira ya saa 12 jioni nilisikia kilio kwa mbali,
wakati najiandaa kwenda, Judith akaja kwangu na kunieleza Edyline
ameanguka na kutoka damu mdomoni, nilipokwenda nilikuta kweli hali hiyo
nikampigia simu mama yake, alipofika tumekuta tayari mtoto amekufa,
lakini tukaamua kumpeleka hospitali na madaktari wakathibitisha
alishafariki muda mrefu,” alisema mama Msuya.
Mmoja wa wanafamilia hiyo aliyesafiri na wazazi wa mtuhumiwa wa mauaji
hayo, alisema haelewi kwa nini baba na mama walishindwa kuhudhuria
mazishini licha ya kuwa walishafika Morogoro.
“Sisi ni wakazi wa Ukerewe, wazazi wa Judith wamefika jana, wamefikia
gesti moja ipo Kichangani wakiwa miongoni mwa watu tisa, lakini sijui
sababu ya wao kushindwa kufika mazishini,” alisema mwanafamilia huyo
huku akiomba hifadhi ya jina lake.
Baba mzazi wa marehemu, Barnabas Mafwere alisema siku ya tukio alikuwa
kazini hivyo hana maelezo marefu, lakini akasema alimchukua mtoto huyo
wa kaka yake ili aishi naye kama mwanaye kabla ya kupokea taarifa za
kitendo chake cha kumnyonga mwanaye.
Akiongoza lbada ya mazishi Padri John Greyson wa Kanisa la Kolla la
Mwili na Damu ya Yesu, aliwaliza watu baada ya kusema marehemu alikuwa
miongoni mwa watoto waliokuwa wapokee Ekaristi Takatifu mwishoni mwa
mwaka huu.
Naye mwakilishi wa Shule ya Kata ya Kolla Hill aliyokuwa akisoma Judith,
Mwalimu Neema Lupena alisema ni jambo la kusikitisha kuwa mtuhumiwa wa
mauaji ni mwanafunzi wao wa kidato cha kwanza, lakini akasema
alipokelewa shuleni hapo licha ya nafasi kujaa kutokana na heshima ya
baba yake mdogo.
Chapisha Maoni