Moja ya story kubwa kwenye siasa za TZ wiki iliyopita ilikuwa ishu ya
CCM kuwafungulia makada wake sita ambao walikiuka kanuni za chama hicho
kwa kutangaza kugombea Urais mapema kinyume na utaratibu wa chama hicho,
mmoja ya waliokuwa wamefungiwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Jana kulikuwa na stori ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba kutangaza
kugombea Urais wa TZ kupitia CCM.. leo Mbunge Edward Lowassa ameongea
kuhusu mambo kadhaa ikiwemo hali ya afya yake, chuki kwenye siasa, na
ujumbe wake kwa CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 TZ.
Ishu ya chuki kwenye siasa >>”Kuna chuki imeibuka kwenye siasa za
nchi yetu na kutakiana mabaya, afya ni neema kutoka kwa Mungu.. mimi
niko sawa kabisa kwa chochote kile.. kwenye Chama chetu waweke utaratibu
tukapimwe wote afya mimi nitakuwa wa kwanza kwenda kupima tuelezane
nani mgonjwa“>> Edward Lowassa.
Sentensi yake nyingine kuhusu tatizo la ajira>>>”Tatizo la
ajira ni bomu lisiposhughulikiwa.. toka nimetoka Serikalini kuna vitu
ambavyo kama tungevifanya kwa kasi ile ambayo tulianza nayo ningepita
napunga mkono nikapata kura zote, hatufanyi maamuzi iwe magumu au
rahisi.. mambo yanakwenda legelege, Rais amefanya jitihada kubwa sana
lakini kuna mambo hayaendi>>> Edward Lowassa.
Suala la elimu>>>”Tukiwekeza vizuri katika elimu tunaweza
kubadilisha nchi yetu.. Tukitaka kuokoa nchi yetu tuwekeze kwenye
elimu“>>> Edward Lowassa.
Kuhama CCM je? >>>”Kuhama chama sina mpango.. nimeingia CCM
toka 1977 sijafanya kazi mahali pengine popote isipokuwa CCM.. My life
is CCM.. huyo ambae hanitaki CCM ndio ahame sio mimi nihame“>>>
Edward Lowassa.
Kauli yake kuhusu visasi >>> “Mimi ni Mkristo, ninaamini kwenye dini yangu sana… sina kisasi na mtu yoyote“>>>
“Upinzani umeanza kupata nguvu kubwa sisi ni chama dola tusibweteke..
wenzetu wanajiandaa vizuri na sisi tujiandae vizuri. Tusifanye mchezo
tusibweteke”>>> MbungeEdward Lowassa.
Credit:Millard ayo.com
Chapisha Maoni