Kocha wa timu ya soka Bournemouth ya
England Eddie Howe ametajwa kuwa meneja bora wa mwaka wa shirikisho la
mameneja wa soka nchini Uingereza LMA.
Kutajwa kwa meneja huyo
kunakuja kufuatia kuiongoza kwa mafanikio klabu yake ambayo imeingia
ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza tokea ianzishwe zaidi ya miaka
100 iliyopita. Howe anakuwa kocha wa pili kutoka nje ya ligi kuu
kushinda tuzo hiyo tangia mwaka 1992. "siamini kabisa, ni jambao
nisilotarajia" alisema kocha huyo.
Chapisha Maoni