
Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia Maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akiwapongeza baadhi ya akinamama waliougua Fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.

Baadhi ya waandishi wa habari wakijitahidi kupata habari katika ukutano huo. (kilonge)

Mmoja wa waathiriwa wa ugonjwa wa Fistula, Lidya Makanda aliyepata matibabu na kupona akionesha kipeperushi kilichookoa maisha yake baada ya kukisoma na kwenda hospitali kutibiwa ugonjwa huo.

Baadhi ya madaktari wanaotoa matibabu ya ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBRT Tanzania wakiwa katika mkutano huo na wanahabari.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja na akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem (kulia) akihojiwa na moja ya wanahabari mara baada ya mkutano huo.

Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV, Sam Mahela (mwenye kipaza sauti cha ITV) akipiga picha na akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya mkutano na wanahabari katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam Tanzania.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
ZAIDI ya
akinamama 3,000 nchini Tanzania huugua ugonjwa wa fistula mara baada ya
kujifungua kila mwaka, huku sababu kubwa ya kupatwa na ugonjwa huo ikiwa
ni huduma duni za afya ya uzazi hasa zile huduma za dharura kwa
wajawazito wanapokuwa wakijifungua.
Taarifa
hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk.
Natalia Kanem alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya
Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani.
Lakini
robotatu ya wagonjwa hao hawana uelewa wa kwamba wanaweza kupata
matibabu na kupona kabisa ugonjwa huo. Ipo haja ya kuongeza bajeti ya
huduma kwa wahusika na kutoa elimu zaidi ili kusaidia jamii hii
inayoangamia kila kukicha kwa matatizo ya fistula. Wakinamama na
wasichana ambao hukumbwa na matatizo ya fistula wamekuwa wakipata
changamoto kubwa baada ya kutengwa na familia zao na wengine kuvunjika
ndoa zao kutokana na hali ya kuvuja mkojo muda wote huku wakitoka na
harufu kali. Alisema ili kuunga mkono juhudi za kukabiliana na ugonjwa
wa fistula.
Hata
hivyo ili kupambana na ugonjwa huo, Dk. Kanen alisema kuanzia mwaka 2003
UNFPA na wadau wenzake ilizinduwa kampeni ya dunia nzima kuhakikisha
inazuia ugonjwa wa fistula (Grobal Campaign to End Fistula) mradi ambao
kwa sasa unafanya kazi kwa zaidi ya mataifa 50 ulimwenguni huku
ukijikita kwa kuzuia, kutibu na kuwasaidia kiuchumi waathirika wa
ugonjwa huo.
Hali hiyo
imewafanya washindwe kujiendeleza katika shughuli zao za kila siku za
kujiongezea kipato, Takribani akinamama 800 wanakufa kila siku dunia
nzima kutokana na matatizo ya uzazi huku 20m kati yao wakijikuta
wameathiriwa vibaya na ugonjwa hatari wa fistula. Inakadiliwa kuwa kati
ya akinamama 50,000 hadi 100,000 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula ni
20,000 tu ndio hufanikiwa kupata matibabu ya ugonjwa huo kwa mwaka.
Kwa
upande wake Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda
Msangi akizungumza na wanahabari kuzungumzia maadhimisho hayo yanayoanza
tarehe 23 Mwezi Mai, 2015 alisema hospitali hiyo na washirika wake
inasapoti maeneo manne ya wagonjwa wa fistula ambayo awali yalionekana
ni changamoto kwao.
Aliyataja
maeneo hayo ni pamoja na Matibabu kwa wagonjwa, Gharama za Usafiri,
Gharama za Chakula na Gharama za Malazi ili kumsaidia mgonjwa kuweza
kukabiliana na changamoto hizo. “…Tunaomba kila mmoja kuanzia ngazi za
familia watoe elimu kwa wahusika waje hospitalini kupata matibabu mapema
kwani ugonjwa huu unatibika,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya
CCBRT, Brenda Msangi. (KILONGE)
Chapisha Maoni