
Maafisa saba wa juu wa shirikisho la soka duniani, FIFA wamekamatwa kwa shutuma za kupokea rushwa. Maafisa
hao walikamatwa kwenye hoteli ya Baur au Lac ya jijini Zurich, Jumatano
hii. Polisi wa Uswisi wamekamata maafisa hao wakiwemo makamu wa rais
wawili baada ya kuivamia kwa kushtukiza hoteli hiyo.

Makamu
wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb anaaminika kuwa mmoja wa maafisa
waliokamatwa alfajiri ya leo wakiwa kwenye hoteli ya kifahari nchini
Uswisi

Eduardo Li, kutoka Costa Rica naye pia alikamatwa kwenye hoteli hiyo ya kifahari
Hatua
hiyo imekuja kufuatia upelelezi uliofanywa na Marekani kwa kipindi cha
miaka mitatu. Waendesha mashtaka wa Marekani wametoa hati za kukamatwa
kwa maofisa 14, kwa madai yakiwemo kutakatisha fedha haramu, ulaghai na
mengine.

Madai hayo ni pamoja na maafisa wa FIFA kupokea rushwa ifikayo dola milioni 150.
Mamlaka
za Uswisi zimefungua upelelezi tofauti wa jinai katika utendaji wa FIFA
kuhusiana na nafasi za kuandaa makombe ya dunia ya mwaka 2018 na 2022
zilizoenda kwa Urusi na Qatar.
Rais wa FIFA Sepp Blatter si miongoni mwa wanaoshtakiwa lakini alikuwa mmoja wa maafisa waliokuwa wakichunguzwa.
Uchaguzi wa FIFA utaendelea kama ulivyopangwa Ijumaa hii na pia michuano ya kombe la dunia nchini Urusi na Qatar haitaathirika.
Chapisha Maoni