Marekani imekiri, kwa mara ya kwanza
kuhusika na mapigano ya anga dhidi ya kikosi cha kiislamu yaliyopelekea
baadhi ya raia kuuawa. Katika mkutano wa dharula Pentagon Mkuu wa
kikosi Luteni Jenerali James Terry ,aliomba radhi kwa mauaji ambayo
yalitokea bila kukusudia na kuua watoto wawili waliouawa wakati wa
machafuko nchini Syria mwaka jana.
Kufuatia tukio lililotokea
mjini Palmyra na Ramadi katika kipindi cha wiki limehusishwa kama kisasi
. Ingawa Rais Barack Obama wa Marekani alisisitiza kuwa Marekani ilikuwa si ya kupoteza
vita na wapiganaji . Rais aliahidi msaada zaidi kwa vikosi vya usalama
nchini Iraq na kusema Marekani itajaribu kuongeza mafunzo ya kijeshi
katika maeneo ya Sunni . Siku moja baada ya mji wa Syria wa Palmyra
kuanguka , Wakazi wa eneo hilo wanasema waislamu wenye siasa kali bado
wanawasaka wale wanaounga mkono serikali.
Hata hivyo wapiganaji wa
Kiislamu wameripotiwa kuwa wengi zaidi ya ulinzi wa eneo la mashariki
mwa Iraq, huku wakijaribu himaya yao huko.
Chapisha Maoni