Polisi wa Mji Mkuu Washington D.C wakifungua rasmi mwendo wa maelfu ya
pikipiki kwaajili ya kutoa heshima kwa wenzao waliofariki wakiwa
wanalihudumia jeshi la nchi hii, katika sikukuu ya mashujaa yaani
‘Memorial Day’ (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Washiriki wa msafara wa Pikipiki unaojulikana kama (Rolling Thunder)
wakipita maeneo ya national mall, Jijini Washington DC katika sherehe za
sikukuu ya Siku ya mashujaa ‘Memorial Day’.
Tukio hilo la kila mwaka la kuwaenzi mashujaa wa kijeshi, kwa mwaka huu
lilianza saa moja asubuhi siku ya Jumapili ya tarehe 24 Mei kwenye eneo
la Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).
Maandamano ya Rolling Thunder (Mtiririko wa Radi) yaliyopewa jina hilo
kutokana na mtiriko wa sauti zitokanazo na injini za mapikipiki,
yaliingia katika eneo la Washington kupitia Daraja la Makumbusho baada
ya kuyajaza maeneo yote ya kuegeshea magari ya Kaskazini na Kusini mwa
Pentagon kwa mapikipiki. Baadaye wapandaji waliendesha kulizunguka eneo
la Mnara wa Makumbusho ya Taifa.
Dogo: Hudhaifa Shatry akipata burudani za msafara wa pikipiki (Rolling
Thunder) Siku ya Jumapili Mei 24, wakati yakipita maeneo ya national
mall, jijini Washington DC
Ingawa maandamano hayo kuchukua muda wa dakika takriban 20 tu tangu
kuanza mpaka kumalizika, hata hvyo, makeke na wingi wa mapikipiki
yanayoshiriki husababisha mabarabara kufungwa kwa karibuni masaa manne.
Mwaka huu barabara zilifungwa kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 9 alasiri.
Wikiendi Ya Siku Ya Mashujaa (Memorial Day Weekend), huadhimishwa
mwishoni mwa Juma la mwisho la mwezi wa Mei kila mwaka nchini Marekani.
Siku yenyewe khaswa ya Mashujaa ni Jumatatu ya mwisho ya Mei, lakini
imepewa jina la "Memorial Day Weekend" kwa vile wafanyakazi wengi hupata
nafasi ya kupumzika kwa siku tatu mfululuzi kuanzia Jumamosi hadi
Jumatatu.
Chapisha Maoni