Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiwaeleza Mawaziri
wa Fedha kuhusu serikali ya Tanzania ilivyonufaika na fedha za Benki ya
Maendeleo katika kutekeleza mipango yake hasa kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete na kushoto kwake ni Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard.
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi
kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa
Fedha kutoka nchini Rwanda,
Ethiophia, Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa
ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.
Waziri
wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa masuala
mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile
ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha
wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.
Kamishna
wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano
yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio katika nchi
za Africa.
Wajumbe
waliohudhuria Mkutano wa Kanda ya Afrika wakimsikiliza na kufuatilia
kwa makini Dkt. Mulu Ketsela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Afrika alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Benki hiyo.
Chapisha Maoni