
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri
ikitokea nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la
Cosafa, baada ya kutolewa katika hatu ya awali ya makundi.
Stars
ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho
baada ya kufungwa bao 1 - 0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote
mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na
Lesotho.
Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars
Mart Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua
hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.
Nooij alisema, mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua
tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B
vimemstajaabisha.
“Mpira wa sasa hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na
matarajio ya kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika
ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij”
Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake
alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha,
anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao
hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania
kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja
wa Borg el Arab jijini Alexandria.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Chapisha Maoni