0











Timu ya Tanzania Taifa Stars

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Olympia Park kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi Swaziland katika michuano ya COSAFA

Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea  na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili na kuongeza kuwa hali ya uwanja iko vizuri. "uwanja una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi changu kufanya mazoezi katika mazingira mazuri" Nooij alisema.

Akizungumzia timu yake katika ufunguzi wa   mashindana hayo dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland utakaochezwa siku ya jumatatu,  kocha huyo amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri, hasa katika mechi ya mwisho wa kirafiki ambapo walitokanao sare hivyo anawaandaa vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.

Timu ya Taifa ya Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi ya nyumbani na wachache wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini. Mchuano huo wa kwanza wa ufunguzi wa COSAFA dhidi ya Taifa Stars na Swaziland utachezwa katika Uwanja wa Olympia Park siku ya jumatatu.

Chapisha Maoni

 
Top