
Kauli hiyo imesemwa na wadau wa sekta ya mifugo na wenyeviti wa
halmashauri kutoka wilaya sita zinazo ongoza kwa migogoro ya ardhi kati
ya wafugaji wakulima na wawekezaji zikiwemo wilaya za
Mvomero,Kiteto,Kilindi,Bunda Serengeti na Simanjiro wanao kutana mkoani
Singida kujadili mbinu za kupunguza migogoro inatokana na makundi hayo
na upatikanaji wa nyanda za malisho na matumizi bora ya Ardhi.
Kwa upande wao wataalam wa kilimo na mifugo kutoka katika
halmashauri hizo wamesema serikali imejitahidi kuchangia sekta hiyo kwa
kupitia miradi ya PADEP na ASDP kauli ambayo imeonesha kuto kubalika na
baadhi ya viongozi wa halmashauri waonalamikia ufinyu wa bajeti katika
sekta hiyo inayo kabiliwa na migogoro kila kukicha.
Nawo watalam wa mifugo kutoka taasisi binafsi wamesema hayo yote
yatawezekana endapo serikali itakuwa tayari kushirikiana na sekta
binafsi na wadau wananguvu kubwa katika kuishiniza serikali.
Chapisha Maoni