
Issa Mnally-GPL
VIBAKA ambao
hawakufahamika mara moja mwishoni mwa wiki iliyopita, walivunja kioo
kidogo cha gari la nyota wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ na
kumkomba vitu mbalimbali vikiwemo power window, kompyuta mpakato na
fedha katika tukio lililotokea Kigamboni, jijini Dar es Salaam.(P.T)

Nyota wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’.
Katika
usiku ambao msanii huyo ilikuwa apande na kufanya shoo katika klabu ya
Kakala, wezi hao walivunja kioo cha gari yake aina ya Verossa yenye
namba T 420 CEP na kufanya uhalifu huo, kitendo kilichosababisha
ashindwe kufanya onyesho hilo.
“Nimelizwa,
roho inauma sana wamechukua na pesa shilingi 35,000 ambazo zilikuwa juu
ya dashbod, wamebakisha elfu tisa tu” alilalamika Tunda Man ambaye
alisema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha Polisi Kigamboni.
Chapisha Maoni