Utawala nchini Malaysia unasema kuwa
umegundua kaburi la pamoja karibu na kambi za kusafirisha watu
kimagendo zilizoachwa karibu na mpaka kati ya nchi hiyo na Thailand.
Ripoti
za vyombo vya habari zinasema kuwa makaburi hayo yaliyogunduliwa wiki
iliyopita huenda yakawa na takriban miili 100 inayokisiwa kuwa ya
wahamiaji kutoka nchini Myanmar na Bangladesh. Waziri wa masuala
ya ndani wa Malaysia aliviambia vyombo vya habari kuwa ameshangazwa
kugundua kuwa huenda kambi hizo zimekuwa eneo hilo kwa miaka mitano.
Mapema mwezi huu makaburi kama hayo yanayoaminika kuwa ya wahamiaji yaligunduliwa eneo lililo kusini mwa Thailand.
Chapisha Maoni