
Viongozi wa Afrika Mashariki wametoa wito kuwa uchaguzi wa Burundi uakhirishwe kwa angalau wiki sita na ghasia zimalizike.
Taarifa hiyo inafuatia mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Uamuzi wa
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kuania muhula wa tatu wa uongozi
katika uchaguzi wa mwezi ujao, umesababisha maandamano kwa majuma kadha
sasa.
Kiongozi wa Burundi hajakuwako kwenye mkutano huo.
Mara ya mwisho alipohudhuria mkutano kama huo awali mwezi May, maafisa wa jeshi walijaribu kumpindua.BBC
Chapisha Maoni