Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akitembelea shamba la ndizi na kahawa la mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji katika kijiji cha Mabila,wilayani Kyerwa mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace
Kubalienda Kishunji ambaye ni mmiliki wa shamba
la Ndizi,, Amesema shamba hilo lina
miche 345 ambayo huvuna magunia 25 na ana shamba la migomba ambalo humpatia
mavuno ya mikungu kwa mwezi 45.
Mzee Kishunji ambaye anaishi katika kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira ameweza kusomesha watoto wawili katika vyuo vikuu vya Dar es salaam na Dodoma na amejenga nyumba ya kisasa yenye thamani kubwa ya fedha kutokana na kilimo bora cha kisasa.
Katibu
Mkuu Kinana yuko ziarani katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Mkulima bora wa migomba na kahawa katika Kijiji cha Mabira, Mzee Eustus
kishunju Ntibalienda (kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, kuhusu alivyoweza kufanikiwa katika kilimo cha mazao hayo, Katibu Mkuu
alipomtembelea mkulima huyo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa
ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Sehemu ya soko la biashara la kisasa na la kimataifa linalojengwa Kigorogoro,mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Katibu
Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana (pichani kati) akiwa ameongozana na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera
Mh.John Mongella wakijadiliana jambo mara baada ya kuzungumza na
wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro,
alipowasili katika kijiji hicho kukagua ujenzi wa soko la kisasa na la
Kimataifa katika kijiji
hicho leo.
Hhata hivyo Kinana ameonesha kusikitishwa baada ya kujulishwa kuwa
ujenzi wa mradi huo, unaohitaji sh. bilioni 1.5 umesimama kutokana na serikali
kuu kukosa fedha.
Kutokana na hali
hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, amesema ni vema miradi muhimu ya maendeleo
iwekwe chini ya usimamizi wa halmashauri ya eneo linalohusika badala ya
serikali kuu.
Amesema, utaratibu wa kuifanya
miradi ya aina hiyo kuwa chini ya usimamizi wa serikali, umekuwa ukileta
matokeo mabaya ikiwemo kusimama kwa ujenzi wa miradi.
Kinana amesema hayo leo,
baada ya kukagua ujenzi wa kitu kikubwa cha biashara, katika Kata ya...
wilayani Kerwa mkoa ni Kagera ambacho ujenzi wake umesimama tangu mwaka juzi
kwa maelezo ya kukosekana fedha.
"Jamani jengo kama hili lilitakiwa
lisimamiwe na Halmashauri ya eneo hili, lakini kusimamiwa na wizara ni kupoteza
muda, hivi kweli ni rahisi mkaguzi atoke Dar es Salaam, kuja hadi huku kukagua
ujenzi tu wa jengo hili, hasa ikizingatiwa kuwa miradi kama hii ni mingi?"
alihoji Kinana.
Wananchi wa
Kijiji cha Kigorogoro katika Kata ya Murongo wilayani Kyerwa mkoani Kagera
wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana akipowasili kuwahutubia
mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Kibingo Wilayani kyerwa mkoani Kagera.
Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimshangilia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,alipopanda jukwaani na kuwasalimia.
Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimsikiliza Katibu Mku wa CCM,Ndgu Kinana alipokuwa akiwahutubia
Katibu Mkuu wa
CCM Abdulrahman Kinana, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
Kibingo, Kata ya Kaisho, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya
CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.
Wananchi wa Kijiji cha Isingiro wakishangilia jambo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa Wilaya
mpya ya Kyerwa,Mh.Edward Ole Lenga,pichani katini Mkuu wa wilaya ya
KaragweMh. Deodatus Kinawiro
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza jambo mara baada ya kupolewa
katika wilaya mpya ya Kyerwa,katika kijiji cha Nkwenda,wilayani humo.
Kabla
ya kuanza ziara yake katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana alianza kazi kwa kuzungumza na wajumbe wa
halmashauri Kuu ya CCm ya wilaya hiyo.
Katibu NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia Wananchi wa kijiji cha Nkwenda,wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha
Nkwenda,Kinana alipita kijijini hapo kuwasalimia wananchi waliokuwa na
shauku kubwa ya kumuona Katibu Mkuu huyo.
Chapisha Maoni