Mbuzi
wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano lililopewa jina la ‘The
Kilitime Stakes’ lililodhaminiwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakati
wa mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Mbuzi
wakishindana katika mbio za ‘the Toyota value+ grand national’ wakati
wa mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi za hisani jijini Dar es
Salaam. Mbio hizo zilikuwa na madhumuni ya kukusanya fedha ili kusaidia
watu wenye mahitaji.
Mwenyekiti wa kamati ya Mbio za Mbuzi, Bi. Karen Stanley akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mashindano hayo.
Washiriki
wa shindano la mavazi wakijinadi ili kujaribu bahati zao. Mbio za mwaka
huu zilikuwa na kauli mbiu ya ‘Bollywood’ambayo ni kiwanda cha filamu
cha India, hivyo washiriki wengi walivaa mavazi yenye asili ya watu wa
nchi hiyo.
Mbuzi wakimalizia mbio zilizoitwa ‘The CBA Sparkers’ wakati wa mashindano hayo zilizodhaminiwa na benki ya CBA.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin (wa tatu kulia) akikabidhi cheti kwa
mwakilishi wa asasi ya KidzCare, Diana Alex wakati wa mashindano ya
mwaka huu ya Mbio za Mbuzi za hisani jijini Dar es Salaam. TBL ilikuwa
wadhamini wa mbio hizo zenye madhumuni ya kukusanya fedha ili kusaidia
watu wenye mahitaji. Wengine kutoka kulia ni Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro, Pamela Kikuli na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla
Thomas.
Mbuzi
wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano lililopewa jina la ‘The
Digital Life’ lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo
wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi jijini Dar es Salaam.
Meneja
Masoko Msaidizi wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Eliavera Timoth
akikabidhi cheti kwa Mwakilishi wa Shule ya Mt. Paulo ya Kibaigwa,
Wilfred Muhogolo (kushoto), ambao ni baadhi ya wanufaika wa fedha
zilizopatikana katika mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi.
JAFO ALITAKA TENA JIMBO LA KISARAWE,AREJESHA FOMU
-
*WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,amerejesha fomu ya
kuomba ridhaa ya kutetea tena Ubunge katika Jimbo la Kisarawe*
*Dkt.Jafo amer...
Chapisha Maoni