
Watafiti katika chuo kikuu nchini
Ausralia wamevumbua mguu wa kwanza bandia duniani wenye uwezo wa
kusisimua hisia halisi za binadamu.
Katika uvumbuzi huo wa Profesa Hubert Egger wa chuo kikuu cha Upper Austria, mguu huo bandia unatumia neva za mwili wa mtu aliyekatwa mguu wake.
Aidha neva za ncha za mguu wa mgonjwa hushikanishwa na waya zinazowasiliana na ubongo kupitia kwa paja.Professor Egger anaelezea kuwa bwana mmoja mlemavu amekuwa akiuvaa mguu huo bandia kwa miezi sita.
Bwana Wolfgang Rangger alisema kuwa katika muda huo wa miezi sita anauwezo wa kubaini iwapo anakanyaga mawe, simiti,na hata nyasi.
''ninapo kanyaga jiwe,nahisi kitu kigumu na pia nikikanyaga mbao,pia najua kuwa kile nilichokanyaga ni tofauti.''''Nimepata maisha mapya baada ya kupokea mguu bandia'' alisema Wolfgang Rangger.

Bwana Wolfgang Rangger amekuwa na mguu huo bandia kwa miezi sita

Chapisha Maoni