Monica
Mbega (kulia) akifurahi pamoja na wana CCM Iringa mjini ambao
walijitokeza kumdhamini kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia
CCM WAKATI mbio za makada wa chama cha mapinduzi (CCM) waliotia nia ya
kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea kushika
kasi kwa kila mgombea kutumia mbinu yake ya kuwafikia wana CCM kuomba
udhamini , aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega leo
ameingia wilaya ya Iringa Mjini mkoani hapa kuomba udhamini na kupata
wajumbe 33 huku akiwataka watanzania kutoaminishwa na mbwembwe za watia
nia wenzake wanazofanya mikoani na kuwa yeye ndie Rais wa awamu ya tano
baada ya Dk Jakaya Kikwete na kuwataka watia nia wenzake wamuunge mkono.
Mbega
ambae alilazimika kusubiri wajumbe 30 wa kumdhamni kwa zaidi ya masaa
manne katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini alitoa kauli hiyo
wakati akizungumza na wanahabari juu ya safari yake hiyo ya kutaka
kwenda Ikulu na kudai kuwa amelazimika kuzuia viongozi wa CCM wilaya ya
Iringa kutomuandalia mbwembwe zozote wala wapambe wa kumshangilia wakati
wa safari yake hiyo ya kutafuta wadhamini.
Alisema
kuwa kuwa anamtegemea Mungu zaidi katika safari yake hiyo ya kwenda
Ikulu na ndio maana hakupenda kuweka makisio ya gharama za safari nzima
ya mchakato huo wa kuelekea kupokea kijiti kwa Rais Dk Kikwete na hivyo
ndio sababu ya yeye kuzunguka bila ya mpambe zaidi ya dereva
anayemuendesha pekee.(P.T)
"Naomba niwaelezeni wazi kuwa sina mgombea wa kumuunga mkono kati ya wote waliojitokeza zaidi ya 30 kwani naamini kuwa namba moja kati ya wote hao waliojitokeza ni Monica Ngenzi Mbega ninasema hivyo kwa kuwa nchi ya sasa inahitaji mwamanke kuongoza kwani mwenye kuweza kuvunja makundi ni mwanamke sio mwanaume tena .....mwanamke ni mwepesi wa kusamehe sio mtu wa makundi hivyo kama hivyo ndivyo ukitanguliza upendo makundi hayatakuwepo. Wapo wenye visasi vya kutoka mwaka 2005 ila sio mimi ....mimi nimetanguliza upendo zaidi....mimi ni mama nitaiunganisha nchi na changamoto inayomkabili Rais wa awamu ya tano ni jinsi na kuiunganisha nchi na mimi ndie pekee wa kuunganisha nchi hii"
Alisema
kuwa iwapo watanzania wataunganishwa kuwa wamoja kuna uwezekano wa nchi
kuachana na utegemezi na hivyo wananchi wake kuwa wamoja na kuweza
kushiriki kujiletea maendeleo yao chini ya rais wao Mbega .
Hivyo
alisema kuwa iwapo chama chake kitamteua na watanzania wakamchagua na
kuingia Ikulu wategemee Tanzania mpya yenye amani ,upendo na mshikamano
na uchumi bora kwa kila mtanzania kuongeza pato binafsi.
Mbega
alisema kuwa tayari Rais wa nchi Dk Kikwete amepata kuueleza umma kuwa
misaada ambayo nchi inapata kutoka kwa wahisani mingine ina masharti
magumu na ndio maana ya baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati
na kuwa iwapo yeye ataingia Ikulu atajaribu kukwepa misaada hiyo na
kulijenga Taifa linalojitegemea lenyewe ili kuto kuwa na miradi isiyo
kamilika kutokana na masharti magumu ya wahisani.
Alisema
kuwa kikubwa kilichomsukuma kuchukua fomu ya kutia nia kuomba kuteuliwa
kuwania Urais ni uzalendo wake katika Taifa wenye shauku la kuliongoza
Taifa la Tanzania kama mwanamke wa kwanza toka nchi ipate uhuru wake
mwaka 1961 bila ya kuongozwa na mwanamke na kudai kuwa hakuna mgombea wa
CCM ambae anajambo lake binafsi la kufanya zaidi ya kutekeleza ilani ya
uchaguzi ya CCM.
"Falsafa yangu ni kusahihisha changamoto zinazoonekana katika kutekeleza ilani hatujaweza kufanikiwa hili ....mheshimiwa Rais Dk Kikwete tunaona jinsi anavyotekeleza ilani katika sekta mbali mbali ila utasikia katika vikao vya kamati kuu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuwa kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ilani hivyo mimi nitaanzia kutekeleza changamoto kwanza .....kwani bajeti inayotengwa ndio inapaswa kusimamiwa kwanza mwelekeo mzima wa serikali yangu ni kuona tunapata Taifa la watu wanaojitegemea wenyewe"
Katika
hatua nyingine Mbega ambaye aliangushwa nafasi ya ubunge mwaka 2010 na
Mbunge Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) alisema kuwa bado ana nguvu ya
kurudi kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini na kumshinda mbunge wa sasa
mchungaji Msigwa kwani bado nguvu za kurejesha jimbo hilo CCM anazo
japo hana mpango wa ubunge zaidi ya kutimiza dhamira yake ya kuingia
Ikulu kama Rais aliyokuwa nayo toka mwaka 2005 na alishindwa kuingia
mwaka 2010 kwa kumheshimu Rais Dr Kikwete pekee ila sasa ni zamu yake.
Pia
alisema CCM bado ina nguvu zaidi katika jimbo la Iringa mjini na
Tanzania kwa ujumla na iwapo suala la upendo likawatangulia watia nia
wote pale wanapokosa kuteuliwa kuungana kwa upendo kumuunga mkono
aliyeteuliwa kamwe suala la wapinzani kushinda litabaki kuwa ni ndoto.
Monica Mbega akisisitiza kuwa hakuna zaidi yake
Monica Mbega akizungumza na wanahabari mjini Iringa leo baada ya kudhaminiwa na wanachama zaidi ya 33
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akitoa taarifa ya idadi ya wana CCM waliomdhamini Mbega
Mbega akifurahia orodha ya wana CCM waliomdhamini
Baadhi ya wadhamini wa Mbega Iringa
Kada wa CCM mama Mwalusamba akimuombea dua Monica Mbega
Monica Mbega akionyesha orodha ya wadhamini wake
Wadhamini wa Mbega Iringa
Hata mimi
nimechukua fomu ya Urais :Naibu meya wa Manispaa ya Iringa ambae ni
diwani wa kata ya Ilala Bw Gervas Ndaki akifurahia kushika mkoba wenye
fomu ya CCM ya kuomba kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, fomu ya Monica Mbega baada ya mgombea huyo kufika
mjini Iringa kusaka wadhamini 30
- Tumeshirikishwa taarifa hiii na Francis Godwon/Matukiodaima Blog
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Monica alisema kuwa endapo atafanikiwa katika kinyang’anyiro hicho, atatekeleza Ilani ya chama na kuendeleza mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne.
‘Nitaangalia changamoto gani ambazo hazikuweza kuleta maendeleo na kuzishughulikia,” alisema. Mbega alisema atafanya hivyo kwa kutumia wataalamu wa ndani ya nchi. Nitatumia watalaamu wa kila aina katika kuiendeleza Tanzania, alisema.
Mbega alisema Serikali ya awamu ya nne imejitahidi kupambana na tatizo la rushwa na yeye akiingia madarakani, ataangalia chanzo cha tatizo hilo na kuongeza nguvu katika hilo.
Mbega alisema hivi sasa tayari vimejitokeza viasharia vya uhasama, mauaji ya albino, wizi, ubaguzi wa dini na ukabila. Alisema ili kuendelea na amani ni lazima kurejesha vitu vinavyojenga amani.
Kwa nini alikosa ubunge?
Alisema siyo kweli wananchi walimkataa, ila utaratibu wa kumpata mgombea ubunge ndani ya CCM, ndiyo ulikua tatizo.
- via MWANANCHI: Monica Mbega ajitosa urais
Chapisha Maoni