Abubakar Katwila 'Q-Chilla' (kulia) akizungumza kuhusiana na ujio wake
mpya katika ukumbi wa Idara ya habari (Maelezo) jijini Dar.
Msanii wa zamani wa muziki wa Bongo fleva, MB DOG, Mkurugenzi wa QS,
Joseph Mhonda ambaye ndiye meneja wao akielezea jambo kwa wanahabari (
hawapo pichani) pamoja na Abubakar Katwila (Q-Chilla).
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abubakar Katwila
‘Q-Chilla’ anatarajia kuzindua nyimbo zake mbili kwa mpigo akiwa ni ujio
wake mpya katika gemu baada ya kupotea kwa muda mrefu.
Meneja mpya wa msanii huyo, Joseph Mhonda ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya QS.Mhonda aliwaomba mashabiki kumpokea katika ujio wake mpya,
akisema kutoweka kwake kulitokana na changamoto nyingi kimuziki.
Kwa upande wake, Q-Chilla mwenyewe alisema sasa amekuja na mabadiliko
mapya kwa kumpata meneja anayetambua na kuthamini mchango wa wasanii,
hivyo atahakikisha jina lake limerudi upya kama zamani.
“Niwahakikishie mashabiki wangu kuwa nimerudi upya katika gemu baada ya
kumpata meneja wangu mpya ambaye anathamini mchango wetu wa kimuziki
hivyo nitahakikisha jina langu linarudi kama zamani”, alisema.
Kesho katika ukumbi wa Hoteli ya Star City, Sinza Afrika Sana jijini Dar
es Salaam, Q Chilla atazindua video mbili za nyimbo zake za For U na
Power of Love ambapo atasindikizwa na wakali mbalimbali wa Bongo Fleva
akiwemo Uwesu Ramadhan ’Amour Genius’ pamoja na Mbwana Mohamed maarufu
kama MB-Dog.
Chapisha Maoni