
Rais wa 9 wa Jamhuri ya Uturuki Suleyman Demirel afariki akiwa na umri wa miaka 91 jijini Ankara
Suleyman Demirel, ambaye alikuwa rais wa 9 wa Jamhuri ya Uturuki, ameripotiwa kufariki kutokana na maradhi ya maradhi ya kupumua na matatizo ya mapigo ya moyo.
Hospitali maalum ya Ankara ilitoa maelezo kuhusiana na kifo cha Suleyman Demirel.
Kwa mujibu wa maelezo hayo yaliyotolewa, Suleyman Demirel alilazwa hospitalini tarehe 13 mwezi Mei mwaka 2015 kutokana na maradhi ya kupumua na matatizo ya mapigo ya moyo.
Matibabu yaliendelea hadi ilipofikia tarehe 16 mwezi Juni mwaka 2015 ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya mno.
Licha ya juhudi zote za matibabu, Suleyman Demirel aliaga dunia tarehe 17 mwezi Juni mwaka 2015 mwendo wa saa 02.05 usiku wa kuamkia Jumatano.
Tunatuma salamu za rambirambi kwa familia yake na jumuiya nzima ya Uturuki, na kumuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema.TRT SWAHILI
Chapisha Maoni