
Shule ya Barclay nchini nchini Uingereza yapiga marufuku kwa wanafunzi waislamu kufunga
Shule ya msingi inayopatikana Barclay nchini Uingereza umewatumia barua wazazi wa wanafunzi kuwafahamisha uamuzi huo ulichukuliwa na shule hiyo.
Shule 4 nchini Uingereza zimefahamisha kuwa hazitowarusu wanafunzi wake kufunga katika mwezi wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza hivi karibu kwa waumini wa dini ya Uislam.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na mmoja wa waasisi katika shule hizo, alifahamisha kwamba katika sheria ya uislam watoto, wazee na wagonjwa hawaruhusiwi kufanga, jambo ambalo lilipelekea shule hizo kupiga marufuku kwa wanafunzi wao kufunga hadi pale watakapofikia umri unaoruhusiwa kufunga na sheria ya Uislam.
Nchini Uingereza zaidi ya masaa 15 ndio waumini hutakiwa kufunga kwa siku jambo ambalo ni vigumu kwa mtoto mdogo kumudu ibada hiyo.
Kwa upande wake, Umoja wa Waislamu nchini Uingereza ulikemea vikali msimamo huo kwa kufahamisha kuwa Uislam haumlazimishi mtoto kufunga na kusema kuwa sheria ya uislam inamlinda mtoto ipasavyo.CHANZO: TRT SWAHILI
Chapisha Maoni