
Mchekeshaji maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Steve Nyerere akifafanua jambo kuhusiana na siasa pamoja na filamu.
Erick Evarist
OHOOO! Mchekeshaji maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedaiwa kupewa fedha za kampeni kutoka kwa wagombea wawili tofauti wa urais 2015, Bernard Membe na Stephen Wasira.
OHOOO! Mchekeshaji maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedaiwa kupewa fedha za kampeni kutoka kwa wagombea wawili tofauti wa urais 2015, Bernard Membe na Stephen Wasira.
Chanzo
makini kimepenyeza ubuyu kuwa, Steve hakuwa na msimamo wa kumfanyia
kampeni mgombea mmoja kwani Jumamosi iliyopita alilipwa na kwenda mkoani
Mwanza kumuunga mkono Wasira alipokuwa anatangaza nia huku pia akiwa
ameweka kibindoni ‘mtonyo’ wa Membe.
“Jamaa
amekula huku na huku. Jumamosi iliyopita aliwachukua wenzake kina JB
(Jacob Steven) na Ray (Vincent Kigosi) wakaenda Mwanza kwa Wasira
kumuunga mkono alipokuwa anatangaza nia. Wakati huohuo amelamba mkwanja
wa Membe ambapo Jumamosi hii (leo) anatarajia kwenda kumuunga mkono
nyumbani kwake Mtama atakapokuwa anatangaza nia,” kilisema chanzo chetu.
Mwanahabari
wetu alimtafuta Steve Nyerere ili kumsikia anazungumziaje suala la yeye
kudaiwa kufanya kampeni kwa wagombea wawili tofauti wakati inaaminika
kabisa msikie alichojibu:
“Watu
wanashindwa kuelewa, Wasira aliniita mimi na wenzangu kama rafiki na si
kazi. Bila hiyana tuliamua kwenda na ndiyo maana pale hutukuzungumza
sababu tulikuwa kama waalikwa wengine.“Kwa Membe hiyo haina kificho,
nitakwenda na wenzangu kama kazi sababu ni kweli namuunga mkono kitambo
tu, si leo wala jana,” alisema Steve Nyerere.
Chapisha Maoni