
Msemaji wa Simba, Hajji Manara
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam-Shaffihdauda
UONGOZI
wa Simba umesema umeamua kulifikisha polisi sakata la usajili wa kiungo
mshambuliaji Ramadhani Singano ‘Messi’ ili kulinda taswira ya klabu
hiyo.
Messi
anadai kutotambua uhalali wa mkataba wake wa miaka mitatu na Simba
uliopo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akisisitiza ana
mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Msimbazi utakaomalizika Julai
Mosi mwaka huu.(P.T)
Hajji
Manara msemaji wa Simba katika mahojiano na moja ya vituo vya redio leo
amesema kuwa kutokana na mvutano ulioibuka baina ya pande zote mbili,
klabu imeona ni vyema kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya dola
ili lipatiwe ufumbuzi.
“Simba ni
taasisi kubwa, suala hili linachafua ‘image’ (taswira) ya taasisi hii.
Tukumbuke pia kwamba Simba ina wadhamini. Inaposemwa kwamba tumeghushi
nyaraka likiwamo dole gumba la Messi ni kashfa kubwa. Wadhamini
wanatuelewaje?” Amehoji Manara bila kutaja lini hasa suala hilo
litatinga polisi.
Wakati
Simba wakitishia kulifikisha suala hilo mikononi mwa polisi tayari Chama
cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) kimeshalifikisha sakata hilo
mikononi mwa TFF ili litatuliwe na Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya shirikisho hilo.
Mwenyekiti
wa Sputanza Mussa Kisoky alisema jijini jana kuwa walifikia hatua ya
kuonana na uongozi wa TFF baada ya kupewa maelezo na winga huyo mwenye
umri wa miaka 21.
Chapisha Maoni