Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akichukua fomu za urais mkoani Dodoma leo.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda leo amechukua fomu ya kuwania kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mhe. Pinda amechukua fomu hiyo katika makao makuu ya chama hicho
yaliyopo mkoani Dodoma ambapo pia alipata fursa ya kuongea na
wanahabari.
Katika mkutano wake na wanahabari amekataa kuelekezea mengi kama
walivyofanya watangaza nia wenzake ili kutoingilia ilani ya chama chake.
Asema ana uzoefu wa uongozi na mafanikio yote ya wizara nchini yeye ndiye kiranja wake.
Apanga kuongeza ukuaji wa uchumi wa pamoja ili kuondoa umbali kati ya mwenye nacho na asiyekuwa nacho.
Chapisha Maoni