0
Waziri Mkuu wa Moldova ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Moldova Kiril Gaburici ajiuzulu baada ya kuhudumu kwa miezi mitatu

Kiril Gaburici, aliyeanza kuhudumu kama waziri mkuu nchini Moldova tarehe 18 mwezi Machi mwaka 2015, ameripotiwa kujiuzulu.

Gaburici alitoa maelezo kwa vyombo vya habari na kutangaza kujiuzulu baada ya kukabiliwa na kesi ya kumiliki vyeti bandia vya elimu.

Gaburici alisisitiza kwamba madai hayo ya umiliki wa vyeti bandia vya elimu ni mbinu ya michezo ya kisiasa inayotumiwa dhidi yake.

Gaburici alisema, ‘’Natumai baada ya kujiuzulu kwangu, tetesi za vyeti vyangu zitaisha na masuala mengine muhimu zaidi yanayokumba jamii yataangaziwa.’’
Wiki iliyopita, Gaburici alitoa maelezo kupitia mtandao wa ofisi ya waziri mkuu na kuwataka baadhi ya viongozi wakuu wa halmashauri kama za nchi kujiuzulu kutokana na madai ya ufisadi.

Gaburici pia alifahamisha kwamba atachukuwa hatua ya kujiuzulu endapo ombi lake halitotiliwa maanani.
Baada ya maelezo hayo, Gaburici mwenye umri wa miaka 38, alianza kuandamwa na kesi za umiliki wa vyeti bandia. CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top