MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA
baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa
baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa
Chuo
kikuu cha IRINGA kesho kinatarajiwa kuadhimisha siku ya utalii wa
kitamaduni katika chuo hicho. Akizungumza na blog hii mkuu wa kitengo
cha utalii cha chuo hicho MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON
SANGA amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo ili kuwakumbusha
wananchi juu ya kuuezi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.
Aidha
SANGA amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikifundisha elimu ya utalii
ndani ya chuo tu sasa imefika wakati wa kutoka na kuifikia moja kwa
moja jamii ambayo haina elimu hiyo.
“Tunaona
wakina mama ntilie wanauza vyakula ya kitamaduni lakini hawana wateja
kwa sababu wanashindwa kutoa huduma ya kuridhisha kwa wateja hata hivyo
mama ntilie wengine hutoa huduma kwa kutofata mazingira ya
kiafya”.alisema SANGA
Ameongeza
kuwa watanzania wengi hatuna tabia ya kuupenda utamaduni wetu au
kuipenda asili yetu tunaona wananchi wengi wanapenda kuiga utamaduni wa
kigeni hivyo tunatakiwa kuuenzi utamaduni wetu.
SANGA amemalizia kwa kuwataka wanachi wajitokeze siku ya jumamosi ili kujionea vitu mbalimbali ya kitamaduni.
Kwa
upande wao WANAFUNZI WA CHUO HICHO hasa wanaosomea masomo ya maliasili
na utalii wamewataka wananchi wa mkoa wa iringa kujitokeza kwa wingi
katika maonyesho hao.
Chapisha Maoni