
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud
Serikali
ya Somalia leo hii itafungua rasmi kesi dhidi ya kenya katika Mahakama
ya kimataifa (ICJ) kufuatia mgogoro wa mpaka baina ya nchi hizo mbili.
Mwandishi
wa BBC wa Idhaa ya Kisomali Mahammud Ali anasema Somalia inailamu kenya
kuwa inamiliki sehemu ya bahari kwa njia isiyo halali.
Mgogoro huu umekuwa ukiendelea kwa miaka sita sasa.
Somalia
inaipeleka Kenya katika mahakama ya kimataifa huko The Hague Uholanzi
kwa madai kwamba kenya imekataa usuluhishi nje ya mahakama.
Somalia na Kenya zinagombea sehemu ya bahari kwa madai kuna mafuta na gesi katika eneo hilo.BBC
Chapisha Maoni