
Wananchi
wakiingia katika banda la Maliasili na Utalii katika Maonesho ya 39 ya
Biashara ya Kimataifa Jijini Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.

Mtaalamu
wa Uenezi Katika Programu ya Panda miti Kibiashara(PFP), George Matiko
akielimisha watu waliotembelea banda la PFP. hilo katika Maonesho ya 39
ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.

Kushoto
ni Afisa misitu Uenezi, Mahendeka Jeremiah (kulia) Afisa Misitu Uenezi
Dorice Nkawamba Wakiwaelimisha washiriki wa maonesho ya sabasaba
waliotembelea banda hilo kuhusu namna ya kujiunga na programu ya Panda
Miti Kibiashara.

Katikati,
ni kiongozi wa banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, Uzeeli Kiangi
akiwa na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Gradness Mkamba (Kuhoto), na
Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa Misitu na nyuki Monica Kyaga (kulia)
walipotembelea banda la Panda la Miti Kibiashara.

Baadhi ya
wananchi wakirudi kutoka katiaka sehemu ya wanyama pori hai ndani ya
banda la Maliasili na Utalii. katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba.

Wananchi wakiwa ndani ya banda la Maliasili na Utalii.

Wananchi
wa Nyanda za Juu Kusini wamefanikiwa kubadili kilimo cha miti kuwa cha
kibiashara baaada ya kupata hamasa kupitia Programu ya PANDA MITI
KIBIASHARA (Private Forestry Programme). Programu hiyo ambayo
ilianzishwa mwaka jana (2014) na serikali za Tanzania na
Finlandimewapatia wananchi mbegu bora za miti ya Misindano na Mikaratusi
na elimu ya kuikuza miti hiyo katikavijiji 12 vya majaribio.
Hayo
yalidhihirika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) katika Banda
la PANDA MITI KIBIASHARA lililomo ndani ya Banda Kuu la Wizara ya
Maliasili na Utalii.
Alipokuwa
anazungumza na watu waliotembelea banda hilo Mtaalam wa Uenezi wa
Programu hiyo Bw George Matiko aliwashauri wananchikupanda miti
kibiasharakama inavyofanyika sasa katika mikoa ya Njombe na Iringa na
sehemu zingine za Nyanda za Juu Kusini.Alisisitiza ‘wakati sasa umefika
wa kuthamini kilimo cha miti na kukuza miti kama zao la biashara’.
Katika
msimu wa mvua wa mwaka huu (2015) miche iliyostawishwa na Programu hiyo
ilipandwa na wananchi katika eneo la zaidi ya hekta 1,000. Kwa kuwa watu
wengi wamehamasika, katika msimu ujao wakupanda miti, vijiji vingi
zaidi vitashirikishwa kwenye Programu hiyo ambapo inategemewa kuwa zaidi
hekta 2,000 zitapandwa miti.
Kwa
kuanzia, Programu hii inafanya shughuli zake katika mikoa ya Njombe
(wilaya za Njombe, Ludewa na Makete), Iringa (wilaya za Mufindi na
Kilolo) na Morogoro (wilaya ya Kilombero).
Lengo kuu
la Programu wa Panda Miti Kibiashara ni kuinua kipato cha wakulima wa
miti kutokana na kupanda miti kibiashara. Programu ya Panda Miti
Kibiashara inahimiza upandaji miti kwa kutumia mbegu bora na kutunza
mashamba kitaalaamhadi miti ifikie umri wa kuvunwa.
Programu
ya Panda Miti Kibishara inashirikiana na Vikundi vya Wakulima wa Miti
(Tree Growers Associations – TGA) pamoja na watu wengine wanaopenda
kupanda miti. Pia Programu hii inatoa misaada ya kupanda miti kwa watu
binafsi na familia zao, wafanya biashara wadogo na wa kati, Taasisi za
umma, vituo vya utafiti, taasisi za elimu, Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali (NGOs) na Asasi za Jamii (CBO).
Vilevile,
ili kuwawezesha wakulima wa miti kujiongezea kipato wakati wakisubiri
miti waliyoipanda ifikie umri wa kuvunwa, Programu inawahimiza wakulima
kufanya Shughuli za Kujiongezea Kipato (Income Generating Activities –
IGA).
Kwa msimu wa mwaka 2015 hadi 2016 wakulima wa miti watapata misaada ya kutekeleza Shughuli za Kujiongezea Kipato zinazohusiana na Ufugaji Nyuki, Kilimo cha Viazi, Kilimo cha Parachichi (Avocado) na kilimo cha Maharage.–
Kwa msimu wa mwaka 2015 hadi 2016 wakulima wa miti watapata misaada ya kutekeleza Shughuli za Kujiongezea Kipato zinazohusiana na Ufugaji Nyuki, Kilimo cha Viazi, Kilimo cha Parachichi (Avocado) na kilimo cha Maharage.–
Chapisha Maoni