ULINZI MKALI KATIKA KAMPENI YA RAIS PIERRE NKURUNZIZA BURUNDI
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aendelea na kampeni yake katika harakati za kugombea kiti cha urais kwa muhula wa 3.
Licha ya kutolewa wito wa kutokuwania kiti cha urais kwa muhula wa 3, rais Pierre Nkurunziza amendesha kampeni tarafani Kabezi, tarafa inayopatikana jijini Bujumbura.
Uchaguzi wa rais nchini Burundi unatarajiwa kufanyika ifikapo Julai 15.
Rais Nkurunziza aliendesha kampeni katika tarafa hiyo chini ya ulinzi mkali ambapo kila baada ya mita 10 kulikuepo na askari anaelinda usalama.
Kulionekana askari wakilinda usalama wakiwa juu ya paa za nyumba pembezuni mwa eneo la kampeni.TRT SWAHILI
Chapisha Maoni