Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao
Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels
Wasanii
wa komedi maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko
yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza
tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.
Wakizungumza
na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa'
wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi
chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala
Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina
hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi
nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.
Baadhi
ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes
Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na
Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali
zaidi zipo katika matengenezo.
Mbali
na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa
wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na
kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na
watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza
na kuimba.
"Kwa
sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni
waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na
kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni
kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.
Pia kupata taarifa zaidi za wasanii wa Komedi Tanzania tembelea mtandao wao wa www.komedizonetz.blogspot.com
Chapisha Maoni