Rais wa FIFA Sepp Blatter na mpinzani wake Ali bin Hussein wa Jordan
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter,anagombea kiti cha
urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika leo
huko Zurich Uswisi.
Uchaguzi huo unaendelea katika kongamano la kila mwaka la shirikisho
hilo licha ya shinikizo kutoka kwa wadau Blatter ajiondoe kufuatia
tuhuma za ufisadi na ulaji rushwa katika shirikisho hilo uliopelekea
maafisa wakuu saba kukamatwa mapema juma hili.
Blatter anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwanamfalme kutoka Jordan Ali Bin al Hussein.
Jinsi kura za urais wa FIFA zilivyogawanywa.
Prince Ali Bin al Hussein ambaye matumaini yake ya kumng'oa madarakani
kiongozi wa muda mrefu Sepp Blatter ilipigwa jeki hapo jana baada ya
rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini kumuunga mkono.
Prince Hussein ameahidi kurejesha hadhi ya shirikisho hilo ambalo
limelaumiwa kwa kuendesha magenge ya ufisadi katika uongozi wake na kura
za uwezenyeji wa kombe la dunia.
Blatter tayari amekana lawama zozote dhidi yake akisema kuwa kwa kweli
sio wajibu wake kuwachunga watu binafsi dhidi ya kushiriki ufisadi.
Maafisa wakuu wa FIFA waliokamatwa
Blatter ambaye amepuuza shinikizo la kumtaka asiwanie urais wa FIFA anasema kuwa ni wakati wa mwanzo mpya katika FIFA.
Blatter ana ufuasi mkubwa miongoni mwa mashirika ya kandanda ya Marekani kusini Afrika na bara Asia.
Mshindi atalazimika kushinda zaidi ya theluthi mbili ya kura za
wanachama zaidi ya mia mbili ilikutawazwa kuwa rais wa shirikisho hilo
moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.
Katika mkondo wa pili yeyote atakayeibuka mshindi ndiye atakaye twaa uongozi wa FIFA.
Chapisha Maoni