Kamishna wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika
majadiliano yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio
katika nchi za Africa.
Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Kanda ya Afrika wakimsikiliza na
kufuatilia kwa makini Dkt. Mulu Ketsela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Afrika alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Benki hiyo.
Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa
masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius
Likwelile ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri
wa Fedha wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha kuhusu serikali ya
Tanzania ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika kutekeleza
mipango yake hasa kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha
wa Rwanda Bw. Claver Gatete na kushoto kwake ni Mchumi Mkuu Rugwabiza
Minega Leonard.
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na
Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchini Rwanda, Ethiophia,
Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya
utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.
Chapisha Maoni