0

Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ametangazwa kuwa mkufunzi bora katika ligi ya Uingereza kwa mara ya tatu. Akihudumia kipindi chake cha pili katika kilabu hiyo rais huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 52 aliiongoza Chelsea kubeba taji lao la kwanza la ligi ya Uingereza katika kipindi cha miaka mitano pamoja na kombe la Ligi.
Kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard ambaye aliifungia Chelsea mabao 20 alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Uingereza msimu huu.

Jose Mourinho.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu ya England kwa msimu huu wa 2014/2015 huku mchezaji wake Eden Hazard akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu.

Eden Hazard.
Hazard amechukua tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu ya England huku akiifungia mabao 14.
Hazard alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wengine saba ambao ni: John Terry, Cesc Fabregas, Nemanja Matic, Sergio Aguero, David de Gea, Harry Kane na Alexis Sanchez.

Chapisha Maoni

 
Top