Mtafiti
Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga
(katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu utafiti uliofanywa
na taasisi hiyo kuhusu viongozi wanaotaka kuwania nafasi ya urais
katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu ambapo Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameonesha kuwapiku wenzake kwa kupata
asilimia 20 akifuatiwa na Dk.Willibrod Slaa aliyepata asilimia 11.7.
Kushoto ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Wakili Mambo na kulia ni
Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Gideon Anyona kutoka Chuo Kikuu cha
Kenyata.
Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
NYOTA
ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa yazidi kung'aa baada utafiti
uliofanywa na Samunge Social Research Center na kugundua wananchi wengi
kumpenda na kumuhitaji agombea urais wa mwaka huu.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi Mtafiti Mkuu wa Tafiti hiyo George Nyaronga
alisema baada ya Waziri huyo kudai kuwa atagombania wananchi wengi
wameonyesha kumuhitaji kwa kiasi kikubwa.
Alisema
katika utafiti huo walioufanya waligundua kuwa Waziri huyo mstaafu
anaongoza kwa asilimia nyingi kuliko wenzake anaowafata.
Akitaja
asilimia hizo alisema Edward Lowassa anaongoza kwa asilimia 20.7
akifuatiwa na Wilbroad Slaa asilimia 11.7, Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia (Chadema)Freeman Mbowe asilimia 3.4, Mwenyekiti wa Chama cha
Wanachi CUF Ibrahim Lipumba asilimia 4.2.
Wengine
ni pamoja na Waziri wa Ujenzi John Magufuli 7.6, Naibu Waziri wa Fedha
Mwigulu Nchemba asilimia 4,Waziri Mkuu Mizengo Pinda asilimia 2.4,Waziri
Mstaafu wa Mambo ya Nje Bernard Membe7.0 na Mwenyekiti wa chama cha
Nccr Mageuzi James Mbatia 1.2.
Alisema
kwa kutokana na nchi kuelekea katika uchaguzi wananchi wamekuwa na
muamko wa hali ya juu katika kuhakikisha kila mmoja atapigapiga kura kwa
mwaka huu.
"Tumefanya
tafiti hizi na kuona kwamba watanzania wengi wameamua kuingia kwenye
masuala ya siasa na kuleta mabadiliko katika nchi yao na si kupigiwa
kura,"alisema.
Alisema
kutokana na utafiti wao wamegundua kuwa wananchi wanahitaji rais ambaye
ni muadilifu, msema ukweli, mwenye afya asiwe na udini wala ukabila na
mzalendo wa nchi yake
Alisema
kutokana na majina hayo ya urais pia katika tafiti zao imeonekana kuwa
vyama vinavyoongoza katika kupendwa na wananchi ni pamoja na Chama cha
Mapinduzi kuonekana kupendwa sana kuliko vyama vyote.
Alivitaja
vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) 53.5,Chama cha
Demokrasia (Chadema) 34.2 ,Chama cha Wazalendo (ACT)1.2 na Umoja wa
Katiba Mpya (Ukawa) 6 na Chama cha wanachi CUF 6. (Imeandaliwa na
mtandao wa www.habari za jamii.com)
Chapisha Maoni