Raia nchini Ethiopia wanapiga kura
hii leo kwenye uchaguzi wa kwanza mkuu tangu kifo cha kiongozi wa muda
mrefu wa nchi hiyo aliyekuwa waziri mkuu Meles Zenawi.
Chama chake kimekuwa madarakani tangu mwaka 1991 na uchumi wa Ethiopia uko katika hali nzuri.
Hata hivyo wapinzani na makundi ya haki za binadamu wanasema kuwa kutokuwepo na uhuru wa kusema ina maana kwamba uchaguzi huo hautakuwa wa haki.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn anatarajiwa kushinda uchaguzi huo
Chapisha Maoni