0







Mahakama moja nchini Misri leo imetoa amri ya kunyongwa kwa aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed Morsi kwa adhabu ya kunyongwa

Mahakama hiyo ilimpata Morsi ambaye aling'olewa madarakani na jeshi mwezi Julai mwaka  2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake mwaka wa 2011.

Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.

Kufuatia uamuzi wa mahakam hiyo  wa kunyongwa kwa Morsi , sasa kauli ya mwisho  itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye  ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi atanyonyongwa au la.

Hata hivyo Sheria za nchi hiyo bado zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.
Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kukutu kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasama wa kisiasa baina yake na uongozi ulioko sasa.
Morsi ambaye aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru  na kuhudumu madarakani kwa mwaka mmoja tu kabla  ya utawala wake kukumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka  amekataa  uhalali wa mahakama iliopo sasa..

Chapisha Maoni

 
Top