Brighton Masalu na Musa Mateja-GPL
SIKU chache
baada ya kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Risasi Jumamosi kuwa staa
wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alibeba mimba na kuzaa
kwa siri huku tetesi zikivuma kuwa baba wa mtoto huyo ni msanii
mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mambo yameanza kunoga baada ya Ray
kufunguka kuwa hahusiki kwa lolote, Risasi Mchanganyiko ‘limemzingira’.
Staa wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
Hivi
karibuni gazeti hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa sasa na
Filamu ya Chicken Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere, Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA ambapo
aliweka wazi.
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...(P.T)
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...(P.T)
kuzungumza
mengi juu ya madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na kwamba watu
wasimtafsiri kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku akimtaja
mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa maisha.
Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo katika jamii na kusisitiza kusiwepo na mjadala unaopingana na kauli zake.
Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo katika jamii na kusisitiza kusiwepo na mjadala unaopingana na kauli zake.
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na mwanaye.
Huku
akiwa amemganda Chuchu kimahaba mbele ya kadamnasi, Ray alikwenda mbele
zaidi na kusema ni jambo la heri kujiweka mbali na watu wanaotafuta
umaarufu kupitia migongo ya watu, kauli iliyozua viulizo kwa waandishi
wetu na yeye kushindwa kuifafanua kwa kile alichokiita ‘hakuwa na mudi
ya mazungumzo zaidi’.
“Achaneni
na hayo mambo, sihusiki kwa lolote na jambo hilo (mtoto) na sipendi
kabisa kuzushiwa mambo kama hayo, watu wasinitafsiri kwa minong’ono na
badala yake wafuate ninachokisema.
“Kwa sasa
mwanamke wa maisha yangu ni huyu (Chuchu) na nitakuwa natembea naye
kila mahali ili kuwafunga midomo wanaojinadi kuwa ni wapenzi wangu,”
alisema Ray huku akiwatazama waandishi wetu kwa macho ya ‘nadhani
mmenielewa sasa’ na kuondoka eneo hilo sanjari na mahabuba wake.
Hivi
karibuni Johari alithibitisha kuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miezi
saba ambaye alimpa jina la Maria linalofanana na la mama wa Ray hivyo
kuibua minong’ono kuwa huenda jamaa huyo anahusika.
Chapisha Maoni