Wasanii wa kizazi kipya Dully Sykes na Shetta Kesho Jumamosi watanogesha katika onyesho la siku ya marafiki wa waziri mkuu mstaaafu na Mbunge wa wilaya Monduli Edward Lowassa itakayofanyika Studio za Tripple A jijini Arusha na kupewa jina kama "Friends of Lowassa Night Party"
Onyesho hilo limeandaliwa na umoja wa Marafiki wa Lowassa Maarufu kama "4 u movement" ambapo tofauti na kuhudhuriwa na Duly & shetta Wasanii wengine wachanga watahudhuria
Kwa mujibu wa Mratibu wa maandalizi ya tukio hilo Jonathan Kassano amesema kuwa lengo la onyesho hilo ni kuwakutanisha marafiki wote wa kiongozi huyo anayetajwa kuwania kiti cha Urais katika Uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka huu ili kufahamiana kubadilishana mawazo na ujuzi.
Jonathan ameeleza kuwa tukio hilo litaendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini ambapo mnamo tarehe 20 May saa 4:00 usiku litafanyika pia Mkoani Dodoma na baadaye jijini Mwanza kabla ya kuenea katika Mikoa mingine.
Mratibu huyo amesema kufanyika kwa onyesho hilo katka Mikoa mbalimbali nchini kutawapa fursa Marafiki wa Lowassa kukutana na kufahamiana.
Chapisha Maoni