
Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa wakazi wa mkoa wa shinyanga,mikoa yote
kanda ya ziwa na mashabiki wetu wote walioko nchi nzima na sehemu
mbalimbali duniani kwa kutoa ushirikiano wao wa dhati kwetu katika
michezo yetu ya ligi kuu tanzania bara msimu wa mwaka 2014-2015
iliomalizika tarehe 9/05/2015.
Tunasema
asanteni sana kwa michango yenu ya hali namali,kifedha,kimawazo na
ushauri pia,na hasa katika kipindi kigumu ambacho tumepitia.
Ulikuwa
ni msimu wetu wa kwanza kushiriki katika ligi mengi tumejifunza na
kuona mazuri na magumu katika ligi hii na soka la tanzania kwa ujumla,
tunaahidi
kuiandaa timu kwa wakati muafaka na kwa weledi mkubwa lengo likiwa ni
kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Tunasisitiza
kuwa bado hatujaanza kushughurika na swala la usajili wa mchezaji
kwasasa na wala hatujafanya mazungumza na mchezaji yoyotekuhusu
kumsajili, tunasubiri ripoti ya mwalimu wetu Mathias Rule kujua
anapendekeza tufanye nini katika kuboresha timu yetu.
Tunakanusha
vikali Taarifa ambazo zinasambaa hivi sasa kuwa tunafanya au tumefanya
mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili kuwasajili akiwemo Juma Kaseja
na Beki wa mtibwa sugar Salim Mbonde hatuna mazungumzo na wachezaji hao
na hatutafanya usajili wowote bila kupata ripoti ya mwalimu.
Kama
ripoti ya mwalimu itaelekeza tufanye usajili tutafanya hivyo na uongozi
umejipanga kufanya usajili wenye tija na umakini wa kutosha kwa manufaa
ya timu yetu ya Stand United fc.
Imetolewa na Idara ya Habari Stand United Fc.
Isaac Edward
Afisa habari.
Chapisha Maoni