WABUNGE
wamesikitishwa kufanya vibaya kwa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars
huku wakitaka makocha wazalendo wapewe nafasi ya kuinoa timu hiyo.
Katika
maoni yake kwenye mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo jana bungeni, wabunge hao wameeleza kuwa,
hali ya michezo nchini ikiwamo soka, inasikitisha.
Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii licha ya kuipongeza Yanga kwa kutwaa
ubingwa wa Tanzania Bara, lakini ilieleza masikitiko yake kuhusu Taifa
Stars.
"Hata
hivyo, Kamati inasikitishwa na timu ya Taifa kufanya vibaya katika
mashindano ya kimataifa. Hivyo, Kamati inaishauri Wizara kuendelea
kuhamasisha wachezaji kujifunza zaidi ili siku nyingine waweze
kupeperusha vizuri bendera ya Taifa," alisema Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Mbunge wa Manyovu, Albert Ntabaliba (CCM).
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni ilieleza kuwa Tanzania imeendelea kuwa kichwa
cha mwendawazimu kuanzia kwenye ngumi, riadha, netiboli, mpira wa kikapu
na kwa kiwango kikubwa kwenye mchezo wa soka.
Msemaji wa Kambi hiyo kwa wizara hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema),
Chapisha Maoni