Urusi imeanza mazoezi makali ya
kivita yanayojumuisha kikosi cha anga cha wanajeshi 150 pamoja nakikosi
cha mashambulio ya mbali ya makombora.
Wizara ya mambo ya ndani ya
Urusi inasema kuwa wanajeshi 12,000 wanatarajiwa kuhusishwa na mazoezi
hayo makali ya siku nne yanayolenga kutaka kujua uimara wa jeshi hilo na
utayari wake. Mazoezi hayo makali yanakuja sawa nay ale
yanayoendeshwa na vikosi vya NATO na majeshi ya Ulaya Nordic
yanayojumuisha zaidi ya wapiganaji 100 wa jeshi la anga.
Hata
hivyo tukio hili la mazoezi ya majeshi ya Urusi yanaleta kwa nchi za
magharibi kufuatia machafuko yanayoendelea Ukraine ambapo Urusi imekuwa
ikinyooshewa kidole kutokana na machafuko hayo.
Chapisha Maoni