Myanmar imesema kuwa jwanamaji wake
wamewaokoa takriban wahamiaji 700 waliokuwa wametelekezwa baharini na
walanguzi wa bianadamu.
Awali maafisa wa mataifa yaliyoko kwenye ukanda huo yalikutana kukubaliana kulipea swala hilo kipao mbele ilikuzuia maafa zaidi baharini.
Hata hivyo maafisa kutoka Myanmar na Umoja wa matafa walikabiliana vikali dhidi ya tuhuma za dhulma dhidi ya watu wa jamii ndogo ya Rohingya.
Naibu kamishena mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, Volker Turk, aliuambia mkutano unaoendelea wa mzozo wa wahamiaji wa bara Asia, kuwa Myanmar inatakikana kuajibikia raia wote wa Nnchi hiyo bila ya kuwabagua wengine.
Taifa hilo haliwatambui watu wa jamii ya Rohingya kama raia wake.
Lakini mjumbe mmoja wa Myanmar Htin Linn, amesema kwamba taifa hilo halipaswi kulaumiwa pekee, ilihali swala zima la ulanguzi wa binadamu ndilo tatizo kuu kwa sasa.
Katika miezi michache iliyopita, maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakimiminika katika pwani ya Indonesia, Malaysia na Thailand huku mamia ya wengine wakiwa bado wamekwama baharini.
Chapisha Maoni