Kata zilizokumbwa na mkasa wa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kata ya
Kibingo inayopa kana na nchi ya Rwanda, kata ya Bugomora na kata ya
Murongo zinazopakana na nchi ya Uganda ambapo wahamiaji haramu zaidi ya
watu 50 wamekamatwa katika zoezi hilo huku afisa muandikishaji jimbo la
Kyerwa Bw.George Mkindo akiwafukuza kazi waandishi wasaidizi kumi
waliosajiliwa kuandikisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuandikisha
wahamiaji haramu kinyume cha sheria za uchaguzi.
Katika haliisiyokuwa ya kawaida mkazi wa kijiji cha Nyamiyaga
ambaye anaishi na mhamiaji haramu kama mke wa ndoa na baadhi ya
mwananchi wamesema kuwa wahamiaji haramu wamehamasishwa na wanasiasa
huku wengine wakitishiwa kufukuzwa nchini endapo wasipojiandikisha
kwenye daftari la kudum la wapiga kura.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Kagera Bw.John Mongela
ameipongeza kamati ya uandikishaji jimbo la Kyewa kwa kudhibiti
wahamiaji haramu waliojipanga kupenyeza kujiandikisha katika daftari la
kudumu ya wapiga kura na kusema kwamba serikali itaimarisha ulinzi
katika maeneo ya mipaka ya nchi.
Chapisha Maoni