Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe akimkabidhi
Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii
hapa Tanzania,katika tamasha la kwanza la Qaswida
lililofanyika
katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na
Kampuni ya Dira ya Mtanzania. PICHA NA MICHUZI JR.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akipokea
tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la
kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha
la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Mh.Bernard
Membe
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza
katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya
Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania
kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu,
Alisema
siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi
iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu
uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa
kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa
viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.
Membe
alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao
kwa nje, wanajinadi wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili
ya dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii
ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi
wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.
“Msikubali
kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na
matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na
dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo
ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama
ukoma.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Chapisha Maoni