13 wafariki katika ajali ya treni iliyozuka nchini Tunisia
Watu 13 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa baada ya treni kugongana nalori katika mji wa Zagwan nchini Tunisia.
Msemaji wa idara ya ulinzi wa raia Al-Manji al-Kadi, alitoa maelezo kwa wanahabari wa AA na kuarifu kuzuka kwa ajali hiyo katika mji wa Zagwan.
Al-Kadi alibainisha kufariki kwa watu 13 na kujeruhiwa kwa wengine 15 katika ajali hiyo.
Ambulansi nyingi ziliwasili katika eneo la tukio na kuwabeba majeruhi kwa ajili ya kuwapeleka hospitalini.
Maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na ajali hiyo.
Soma pia CHANZO TRT SWAHILI
Chapisha Maoni