Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New
York, Mhe.Balozi Ramadhani Mwinyi pamoja na mama mwenye nyumba wake
wakiwa na tabasamu la bashasha baada ya Iftar nyumbani kwao New
Rochelle. NY. Mama mwenye nyumba wa balozi pamoja na mume wake
waliwakaribisha Watanzania wa jumuiya ya New York nyumbani kwao na
kufuturu nao pamoja.
Akina mama wa jumuiya ya Watanzania wa New York wakijiandalia chakula.
Akina mama walikuja na familia zao kama unavyoona kwenye ukodak huu wa Vijimambo.
Mh. Balozi Mwinyi pamoja na mama mwenye nyumba wake wameandaa
utaratibu huu wa kufuturu pamoja na wanajumuiya kila wiki endi ndani
ya mfungo huu wa Ramadhani.
Akina baba nao wakijiandalia chakula kama unavyoona kwenye ukodak huu hapa mbele yako.
Kama kawaida yake Mhe. Balozi akitoa shukrani mbele ya wageni wake
kwa kuitikia mwaliko wake na kujumuika nae kwa Iftar nyumbani kwake.
Kwa picha zaidi nenda soma zaidi.
Chapisha Maoni