Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado ziko. Anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.
Kama mwanachama cha ICC, Afrika Kusini inastahli kumkamata Bashir ikiwa atasafiri kwenda nchin humo . Lakini Muungano wa Afrika umekataa kushirikiana na mahakama hiyo ya kimataifa ukisema kuwa ICC inawaonea viongozi wa Afrika. CHANZO: BBC SWAHILI
Chapisha Maoni