Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizokuwa za
wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na vyama vingine mara
baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu mkoani
Mwanza.
Katibu
Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la
CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na
Chama cha Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi9 ya mkoa Mwanza
akimalizia mkoa wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya
Tanzania Bara na Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa
nchini na nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.Kinana
amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku
akihimiza uhai wa CCM ambapo pia katika ziara hiyo amekuwa akiongozana
na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi.
Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni
Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw.
Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao na Bi.
Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA.(VICTOR)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw.
Miraji Mtaturu wakiwa tayari kupokea kadi za wananchi waliokuwa
wanachama wa vyama mbalimbali wakati alipojiunga na CCM kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika Kisesa wilayani Magu leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi hizo kutoka kwa
wananchi hao kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu
Magesa Mulongo wakifungua maji kama ishara uazinduzi wa utumiaji wa maji
hayo katika mji wa Magu.
Baadhi ya wananchi wakisubiri kuchota maji mara baada ya uzinduzi huo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati
alipozindua kikundi cha wajasiriamali cha Magu alipokitembelea leo.
Mwenyekiti
wa CCM mkoani Mwanza Ndugu Anthony Diallo akisalimia wajumbe wa mkutano
mkuu wa jimbo uliofanyika kwenye ukumbi wa CCM mjini Magu
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano kabla ya Katibu Mkuu Kinana kusalimia wananchi mjini Magu.
Kwaya ya Magu One Thietre kikiimba wimbo maalum katika mkutano huo wa kusalimia wananchi mjini Magu.
Mkuu wa
mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu
kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda
katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za
uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya
moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana
kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua wa nyumba hiyo katika
kijiji cha Irungu wilayani magu akiwa ameongozana na Mkuu wa mkoa wa
Mwanza Ndugu Magesa Mulongo kushoto.
Chapisha Maoni