Nyota wa R&B, Maria Carey akiwa na bilionea, James Packer.
CANNES, Ufaransa
HISIA ni
kitu kingine! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya nyota wa R&B, Maria
Carey, 45, kunasa katika penzi la bilionea, James Packer, 47, raia wa
Australia.
Maria,
aliwahi kuolewa na Nick Cannon lakini waliachana Agosti mwaka jana kwa
talaka baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa miaka sita wakiwa na watoto
wawili mapacha.
Taarifa
ni kwamba hivi sasa mwanamama huyo mrembo amenasa kwenye penzi la
bilionea huyo kijana. Imeripotiwa kuwa, Maria na James wamekuwa karibu
na wamekuwa wakionekana pamoja wakila raha huku wakionekana sehemu
mbalimbali kama Casino, migahawani na kwenye boti wakiwa wameshikana
mikono kimahaba. (DK)
Bilionea huyo ameripotiwa na Jarida la Forbes kuwa anashika namba nne kwa utajiri nchini Australia.
Chapisha Maoni