Imeripotiwa kutoka mkoani Simiyu katika Wilaya ya Bariadi kuwa Mkuu wa
Wilaya (DC) hiyo Bw. Ponsian Nyami amemuomba Rais Jakaya Kikwete
asimwonee huruma na badala yake atengue uteuzi wake kwa maana ameshindwa
kusimamia ujenzi wa maabara katika wilaya yake.
Kabla ya kauli ya Nyami, Mbwilo alitoa lawama kwa DC kwa kushindwa
kusimamia ipasavyo agizo la Rais na kueleza kuwa ndani ya Mkoa, Wilaya
hiyo ndiyo ya mwisho katika utekelezaji wa agizo husika.
Hata hivyo Mkuu huyo mkoa alisema kuwa viongozi pamoja na watendaji
wameshindwa kutekeleza agizo hilo ikiwa pamoja na miundombinu hasa
barabara ndani ya wilaya hiyo kuwa chini ya kiwango, ambapo alimtaka
Mkuu wa wilaya kuwachukulia hatua watumishi wote walisababisha hali
hiyo.
Hata hivyo, Katibu Tawala wa Mkoa naye aliutupia lawama uongozi wa
Wilaya hiyo kwa kushindwa uwajibka, huku akieleza kuwa maabara
zilizojengwa ziko chini ya kiwango.
Baada ya viongonzi hao kuongea, Mkuu wa Wilaya, Nyami alisema:
“Namuunga mkono Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa. Ni kweli tumefanya
vibaya, makosa haya ni makosa yangu mimi na wala sina haja ya kuomba
msamaha. Niko tayari kuwajibishwa kwa lolote lile na kwa wakati wowote
maana nilipoteuliwa nilihaidi kuwa nitaisimamia na kuiheshimu, sasa
naona nimeshindwa na usinionee huruma. Nakiri nimeshindwa.”
Nyami alibainisha kuwa yeye kama kiongozi Mkuu ndani ya wilaya hiyo
haoni haja ya kuonewa huruma, kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi huo
ikiwa pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Chapisha Maoni